Basi la Kampuni ya Wibonela lapinduka Asubuhi ya leo Kahama, phantom
WATU
kadhaa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa asubuhi hii kwenye
ajali ya basi la Wibonela lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar
lililopinduka eneo la kona ya Phantom, Kahama.
Chanzo cha ajali hiyo
ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa kulimudu lilipofika
kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia mtaroni na kupinduka.
Idadi kamili ya waliopoteza maisha na majeruhi kwenye ajali hiyo bado haijafahamika.
Baadhi
ya miili tayari imetolewa katika eneo la ajali huku majeruhi nao
wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Wilaya Kahama kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment